Serikali imesema inaboresha huduma za upatikanaji wa vyeti kwa kukamilisha utaratibu wa kuhama kutoka kwenye mfumo wa vyeti vya makaratasi/vitabu na kwenda kwenye mfumo wa vyeti vya kidijitali (Covid-19 Vaccine Electronic Certificates).
Kadi maalum za kieletroniki zinazoendelea kuandaliwa zitakuwa na vigezo vya kimataifa vya uthibitisho wa kupata chanjo ambapo vigezo hivyo ni pamoja na kuwa na utambulisho wa siri ambayo itajumuisha taarifa za mpokeaji chanjo, chanjo aliyopata, muda na mahali alipopata chanjo husika.
Tangu kuanza kwa zoezi la uchanjaji Agosti 3, rekodi ya makundi ya walengwa peke yake kufikia Agosti 7 ilionyesha zaidi 164,500 walikuwa wameshajiandikisha (booking) kwa ajili ya kupatiwa chanjo wiki hii huku wengine 105,745 wakiwa tayari wamechanjwa.