Tunakumbuka ajali ya basi la Wanafunzi wa Lucky Vincent iliyotokea Karatu, Arusha na kuua 32 na kuacha Majeruhi watatu ambao wanatibiwa kwenye Hospitali ya Mercy, Sioux City Iowa, Marekani huku Mmiliki wa shule hiyo na Makamu Mkuu wa Shule wakishikiliwa na Polisi.
Sasa new story leo July 5, 2017 ni kwamba Mahakama ya Wilaya Arusha imesema kuwa Upelelezi wa kesi inayomkabili mmiliki wa Shule ya Lucky Vincent, Innocent Mosha na Makamu Mkuu wa Shule hiyo Longino Vincent umekamilika na kesi hiyo itaanza kusikilizwa July 26, 2017 wakikabiliwa na mashtaka matano.
Mashtaka wanayokabiliwa nayo pamoja na Mmiliki huyo kuruhusu Dereva kuendesha gari la abiria bila kuwa na leseni ya usafirishaji, kutumia gari bila kuwa na BIMA pamoja na kushindwa kuingia mkataba na Mwajiriwa.
Mashtaka mengine ni kuzidisha abiria 13 kwenye gari pamoja Kaimu Mkuu wa Shule kuratibu safari na kuruhusu gari kuzidisha abiria.
VIDEO: Hivi karibuni Bunge lilitangazwa kutenga chumba maaum kwa ajili ya Wabunge wanawake wenye watoto wachanga kukitumia chumba hicho kuwanyonyeshea watoto wao…Sheria ya Tanzania ikoje kwenye mambo kama hayo? Huyu Mwanasheria Jebra Kambole anajibu…bonyeza PLAY kwenye hii VIDEO kutazama!!!