Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Professor Joyce Ndalichako alivunja bodi ya Tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU), baada ya kubaini kuwa tume hiyo ilipitisha majina ya wanafunzi 486 wasio na sifa kusomea Shahada ya Elimu.
Professor Ndalichako alitangaza uamuzi huo ikiwa ni pamoja na kuwasimamisha kazi baadhi ya Maafisa wa Tume hiyo waliobainika kushindwa kutekeleza wajibu wao.
Miongoni mwa waliosimamishwa kazi pia yupo aliyekuwa katibu mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Professor Yunus Mgaya ambaye leo alikutana na vyombo vya habari kueleza jinsi hakupendezwa na taarifa hizo namna watu walivyokuwa wakiziandika katika mitandao mbalimbali.
‘Nimesikitishwa na taarifa zilizoandikwa katika vyombo mbalimbali vya habari hususani magazeti kuhusu taarifa zilizotolewa na Waziri wa Elimu nisingependa kuzungumza mengi ila tume inaendelea na uchaguzi wa taarifa hizo kwahiyo nawashauri vyombo vya habari kuzingatia kanuni za taalamu zao kufikisha habari zilizosahihi katika jamii’–Professor Yunus
ULIKOSA HII YA FREEMAN MBOWE KUZUNGUMZA BAADA YA UPINZANI KUTOLEWA TENA BUNGENI/ UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE