Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya story ambayo imeandikwa June 10 2016 kwenye gazeti la Mtanzania ni hii yenye kichwa cha habari ‘Wapinzani wamjibu Naibu Spika Dk Tulia’
Gazeti hilo limeripoti kuwa wabunge wa kambi rasmi ya upinzani bungeni wamebeza uamuzi uliofanywa na Naibu Spika Dk. Tulia Ackson kwa kusitisha posho zao na kusema hawakwenda Bungeni kufuata malipo hayo.
Kupitia gazeti hilo limenukuu kauli mbalimbali za wabunge wa upinzani wakibeza uamuzi huo wa Naibu Spika, Gazeti hilo limemnukuu David Silinde akisema…….>>> Kauli ya kusitishwa kwa posho za wabunge wa upinzani eti kwa sababu wanatoka kwenye ukumbi wa bunge ni ishara tosha kuwa hajatulia na anakurupuka lakini uamuzi wake huo hautukatishi tamaa wa kuendelea na msimamo wetu dhidi yake’
Gazeti hilo limemnukuu pia Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi ……>>> kuhusu hilo suala la posho kwetu sisi si lolote tutaendelea kufanya kazi tuliyotumwa na wananchi kwa kutetea masilahi yao na wala hatukufuata posho’
Gazeti hili pia lilizungumza na Kiongozi wa Kambi rasmi ya upinzani bungeni Freeman Mbowe ambapo alisema…….>>>Nimeshangazwa na uamuzi na Naibu Spika ndani ya siku tatu kwa jambo moja ametoa uamuzi unaotofautiana, kwanza alieleza kanuni haziruhusu kukatwa posho wabunge jana anasema ameangalia kanuni zinaruhusu iweje mtu mmoja ajipinge mwenyewe’
#MTANZANIA Wapinzani wamebeza uamuzi wa Naibu Spika wa kusitisha posho na kusema hawakwenda bungeni kufuata posho pic.twitter.com/4wZSHduwX0
— millardayo (@millardayo) June 10, 2016
#MWANANNCHI CHADEMA wajifungia kutwa nzima kujadili hatua za kuchukua dhidi ya kitendo cha polisi kuzuia mikutano pic.twitter.com/PBs6u8dHI1
— millardayo (@millardayo) June 10, 2016
#MWANANCHI Dk Mpango apigwa chenga baada ya kusema Kenya inatoza VAT ktk utalii, lakini tayari imefuta kodi hiyo pic.twitter.com/QWjjiGpq72
— millardayo (@millardayo) June 10, 2016
#MWANANCHI Watanzania 495 waliokwama India wataibebesha Serikali mil 289.7 kwa ajili ya kuwarejesha nyumbani pic.twitter.com/QlE8ZiGq3w
— millardayo (@millardayo) June 10, 2016
#MWANANCHI Mkurugenzi wa Mashtaka 'DPP' ameshinda rufaa dhidi ya Harry Kitilya, Shose Sinare na Sioi Solomoni pic.twitter.com/N699DNvav5
— millardayo (@millardayo) June 10, 2016
#MWANANCHI Watumishi hewa 170 waliobainika March hadi June 2016 Mbeya wameisababishia serikali hasara ya mil 773.8 pic.twitter.com/LP7evezzAc
— millardayo (@millardayo) June 10, 2016
#MWANANCHI Rais mstaafu Mwinyi ameishauri UDART kuongeza mabasi ya wanafunzi na mengine ya wazi juu ya watalii pic.twitter.com/D39QMtNOQP
— millardayo (@millardayo) June 10, 2016
#MWANANCHI BoT imeacha kuchapisha noti ya 500 kwa ajili ya kuiondoa kwenye mzunguko na kuiwezesha sarafu ya 500 pic.twitter.com/kIN6oBgbfu
— millardayo (@millardayo) June 10, 2016
#NIPASHE Abiria wa mabasi ya haraka wanatarajia kuanza kutumia kadi za kielektroniki wiki ijayo pic.twitter.com/OrCogVzWGT
— millardayo (@millardayo) June 10, 2016
#NIPASHE Ilala yapiga marufuku kampuni za kibiashara kupaka rangi na kuweka matangazo ktk majengo bila kupata kibali pic.twitter.com/otVtFkf9Hn
— millardayo (@millardayo) June 10, 2016
#MAJIRA Ilala imeagiza wamiliki wa majengo yaliyochakaa kuyapaka rangi na kuweka taa ili kuimarisha ulinzi pic.twitter.com/MzdFes1eB6
— millardayo (@millardayo) June 10, 2016
#RaiaTANZANIA Watanzania washauriwa kutoenda nje bila mikataba ya ajira ambayo wameielewa pia imeandikwa Kiswahili pic.twitter.com/LZe6gqkgzF
— millardayo (@millardayo) June 10, 2016
#JamboLEO Serikali yazidi kubana wanaoingiza sukari kwa kuweka mpango utakaopandisha ushuru kila mwaka wa fedha pic.twitter.com/7I1hUj52Rs
— millardayo (@millardayo) June 10, 2016
#JamboLEO Serikali imeanza msako kwa watu wanaohusika na mtandao wa biashara ya kuuza wasichana nchi za Asia pic.twitter.com/27lIYg5v5m
— millardayo (@millardayo) June 10, 2016
#JamboLEO Serikali imefuta ushuru wa kuingiza vifaa vya matumizi ya hospitali, ikiwamo majokofu ya kuhifadhi maiti pic.twitter.com/2gpIlOv2UO
— millardayo (@millardayo) June 10, 2016
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI KUTOKA AYO TV JUNE 10 2016? UNAWEZA KUTAZAMA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE