Wadhamini wa aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu wamewasilisha maombi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya kutaka Lissu akamatwe kwasababu wao wameshindwa “tumeshindwa kumpata kwa nguvu zetu”.
Kutokana na hatua hiyo, Wakili Wankyo Simon ameiomba Mahakama iahirishe kesi hiyo hadi siku nyingine na Hakimu Simba ameahirisha kesi hadi February 21, 2020 ili kuangalia sheria inasemaje kuhusu maombi ya wadhamini hao.
Mbali na Lissu washitakiwa wengine ni Simon Mkina, Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehboob ambapo kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka ya uchochezi.