Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) ya miradi ya maendeleo inaeleza kuwa wafanyakazi wa kigeni 1,538 kati ya wafanyakazi 2,408 wa kigeni wanaojenga reli ya kisasa kipande cha kwanza na cha pili kutoka DSM hawakuwa na vibali vya kazi.
“Mapitio ya ripoti ya maendeleo ya kazi ya mwezi wa Novemba 2020 yalibaini kuwa jumla ya raia wa kigeni 586 kati ya 924 walioajiriwa kwenye kipande cha kwanza cha ujenzi wa reli ya kisasa hawakuwa na vibali vya kufanya kazi.” CAG
“Hali hii pia ilibainika kwenye kipande cha ujenzi cha pili ambapo ilibainika kuwa jumla ya raia wa kigeni 952 kati ya 1,484 hawakuwa na vibali vya kufanya kazi,” inaeleza ripoti hiyo ya miradi ya maendeleo” CAG
“Mahojiano zaidi na maafisa wa TRC (Shirika la Reli Tanzania) yalionesha kuwa idara ya uhamiaji ilitoa idhini ya raia hao wa kigeni kutumia visa ya biashara kuendelea kufanya kazi wakati maombi yao ya vibali vya kazi yakishughulikiwa.” CAG