Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Pwani imewakamata wahamiaji haramu 54 kutoka Ethiopia ambao waliokuwa wanasafirishwa katika lori ya mizigo lililobeba magodoro kutoka Bagamoyo na kukamatiwa Msola Chalinze Mkoa wa Pwani.
Hayo ameyaeleza Afisa Uhamiaji Mkoa wa Pwani Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Omary Hassani mara baada ya kukamta lori aina ya Scania lenye namba za usajili T 191 AYD lililokua linaelekea Tunduma Mkoa wa Songwe huku likiwa limewaficha Wahamiaji haramu katikati ya magodoro ambayo yaliwekwa mlangoni kuwaficha wasionekane na wanamshikilia dereva wa lori hilo na wakala wa kusafirisha watu hao.
Aidha Kamishna Msaidizi Omary amesema kufanikiwa kuwakamata Wahamiaji haramu hao ni ushirikiano baina ya idara ya uhamiaji Mkoa wa Pwani na Polisi Mkoa huo ambao wote wanaendesha operation za kuwatafuta watu hao kuwafikisha Mahakamani.