Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Mwita Waitara amefanya kikao na Menejimenti ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) pamoja na kufanya ziara ya kutembelea Mradi wa nyumba za Makazi za Magomeni Kota ambapo TBA ni Mkandarasi na Mshauri Elekezi.
“Nilipoenda Arusha kiukweli ule mradi ni mzuri sana nawapongeza lakini pia nawapongeza yale magorofa hayajawahi kujengwa Tanzania kwahiyo yakikamilika yatakuwa majengo ya mfano , nawapongeza sana mradi ule mnajenga kwa fedha za ndani na nyie hamna tuhuma ya kujengo kwa kiwango kile hongereni- Waitara
“Na mimi nilipokuja mwanzoni kwenye hii Wizara nilikuwa nawachukia sana nataka kusema ukweli , sasa miradi ikichelewa mnatakiwa mtoe Elimu mtu anatakiwa kujua Halmashauri fulani kwanini mradi umechelewa na usiposema basi mzigo wote wa lawama utakuhusu”- Waitara
JAMAA ARUSHA AJITEKA NA KUJIUMIZA ILI APATE MILIONI TATU ALIPE MADENI