Oktoba 4, 2020 Mbunge aliyepita bila kupingwa Jimbo la Ludewa kupitia chama cha mapinduzi CCM Wakili Msomi Joseph Kamonga amesema Dr John Pombe Magufuli anapaswa kupewa ridhaa na Wana-Ludewa kuiongoza tena nchi yetu kutokana na mambo ambayo ameyafanya na anayotaka kufunya katika Jimbo la Ludewa.
Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kipingu kinacho kutikana katika kata ya Ruhuhu wakili Joseph Kamonga Amesema rais magufuli amefanya kazi nzuri sana tanzania na hata Ludewa ” Rais wetu mpendwa ameanza kutujengea Daraja la Mto Ruhuhu ili kuokoa maisha yetu kwani wengi walikuwa wakipoteza maisha pale , ameanza kujenga Barabara kilomita hamsini kwa kiwango cha Mege kutoka Lusitu hadi mawengi , ametoa shilingi bilioni 167.5 kwaajili ya ujenzi wa lami kwa kiwango cha Zege ili kuimarisha Uchumi wetu”. Wakili Kamonga
Hata hivyo amesema kwa kutambua umuhimu wa Elimu , Rais Magufuli aliamua kutoa Elimu bila malipo kuanzia Shule ya Msingi hadi Sekondari na endapo mtampa ridhaa ya kuwa Rais kwa mara nyingine tena basi ameahidi kutoa Elimu bila malipo hadi Kidato cha Sita na changamoto za upungufu wa Walimu na Vyumba vya Madarasa kwa baadhi ya Shule vyote vitafanyiwa Kazi.
“Ndugu zangu katika vijiji mbalimbali nilivyotembelea katika Tarafa ya Masasi nimekuwa nikielezwa juu ya changamoto ya upungufu wa Walimu katika Shule zetu za Msingi , niwahakikishie ndugu zangu tatizo hili litafanyiwa kazi na litakwisha ”. Wakili Kamonga
Kwa upande wa Afya wakili Kamonga amesema Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli imefanikiwa kujenga Zahanati lakini ataendelea kufuatilia kuhakikisha Madawa na Wahudumu wanaongezeka ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za Afya.
Katika hatua nyingine Wakili Kamonga amesema anafahamu Vipaji vya Michezo , Utamaduni na Sanaa vinavyopatikana katika Tarafa ya Masasi na amewahakikishia Wananchi wa Vijiji vya Kipingu, Ngelenge na Lihagule kuwa Sekta hiyo ataitazama kwa ukaribu ili kutoa Fursa Mpya za Ajira.
”Tarafa hii ilikuwa inatoa wachezaji wazuri sana wa mpira kwahiyo tutaboresha Sekta ya michezo kwani Michezo ni Ajira lakini pia inajenga Afya na michezo itakwenda pamoja na utamaduni , kama kutakuwa na mashindano sehemu yeyote huko tutakwenda kushindana ” , Wakili Kamonga amemaliza kwa kuwasisitiza Wananchi wa Tarafa ya Masasi kujitokeza kuwapigia kura Viongozi wa CCM hapo Oktoba 28.