Kundi la kigaidi la ISIS limedai kuhusika na shambulizi lililowaua Watu 40 na kujeruhi wengine zaidi ya 100 Nchini Urusi usiku huu baada ya Watu wenye silaha ambao wameficha sura zao (kininja) kuwashambulia kwa risasi Watu ambao walikuwa kwenye Tamasha katika eneo la Crocus City Hall ambalo hutumika kwa shughuli za muziki na kuna maduka yanayouza bidhaa mbalimbali karibu na Mji Mkuu, Moscow ambapo pia wamelipua eneo hilo na kusababisha moto mkubwa.
CNN imeripoti kuwa kundi hilo limetoa taarifa ya kuhusika na shambulizi hilo kupitia ujumbe mfupi uliochapishwa kwenye mtandao wa Telegram na Chombo cha Habari kinachotumiwa na kundi hilo cha Amaq.