Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli ametuma salam za rambirambi kwa uongozi wa Shule ya Byamungu Islamic iliyopo Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera, Wazazi, ndugu jamaa na marafiki kufuatia vifo vya watoto 10 waliopoteza maisha kwa ajali ya moto na saba kujeruhiwa.
Moto huo ambao chanzo chake hakijajulikana, umetokea usiku wa kuamkia leo katika bweni la wavulana.
“Nimesikitika sana na taarifa za watoto 10 kufariki kwa moto shuleni Byamungu, naombeni wote tusimame tuziombee roho za marehemu zipumzike kwa amani,” Rais Magufuli