Kiukweli Tanzania tunajitahidi sana kwa kuwekeza kwenye elimu na kuhakikisha watoto wetu wanafikia malengo katika maisha yao
Lakini ziko baadhi ya shule haswa zilizopo Vijijini bado zinahitaji nguvu za ziada katika kuboresha elimu na mazingira kwa ujumla, Leo Mtu wangu nimetembelea katika Wilaya ya Namtumbo iliyoko Mkoani Ruvuma nikakutana na hii shule ya Msingi Namtumbo yenye wanafunzi 695 na walimu 19 mazingira ya shule bado hayavutii na chakushangaza zaidi shule ina choo kimoja tu! na nyumba tatu za walimu na mpaka sasa walibu bado hawajajengewa choo..