Mkuu wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Julius Mtatiro ameendeleza oparesheni ya kuwafuatilia watoto walioko majumbani wakati huu wa likizo ya corona na kubaini Watoto wawili wakiwa wanaishi kama Mke na Mume, Watoto hao ambao majina yao yamehifadhiwa wanasoma darasa la saba katika Shule ya Msingi Mchangani kata ya Mchangani, Tunduru.
Mtatiro amekutana na Wazazi wa Watoto hao pamoja na Watoto wenyewe na ametoa adhabu ya viboko kwa Mtoto wa kiume na kumnyoa nywele hadharani pamoja na hatua nyingine za kisheria ikiwemo kuendelea kumshikilia.
DC Mtatiro ameelekeza Wazazi wa Watoto hao washitakiwe mara moja kwasababu kuja ushahidi wa wazi kuwa walikula njama na kuwaruhusu Watoto hao waishi kinyumba na hata kuwapangishia nyumba ambayo watoto hao wameendelea kuishi kama Mke na Mume wakati huu ambapo shule zimefungwa.