Wananchi katika kitongoji cha Rutozo Kata ya Katoro Halmashauri ya Wilaya ya Geita Mkoani Geita wamevuruga Mkutano wa hadhara kwa kile kinachomtuhumu Mwenyekiti wa kitongoji hicho kushindwa kusoma mapato na Matumizi ya Baadhi ya Miradi ambayo imeshindwa kumalizika kwa kipindi cha muda mrefu.
Wakizungumza Mbele ya waandishi wa habari wananchi hao wamesema katika maeneo yao wamekuwa wakichangishwa fedha kwa ajili ya Ujenzi wa Miradi mbalimbali ambayo imeshindwa kumalizika huku wakidai Mwenyekiti ambaye amekuwa akishiriki zoezi hilo kuwapa sababu za nini kinachopelekea miradi hiyo kutomalizika kwa uharaka.