Kamanda wa jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa amesema jeshi la polisi mkoani humo, linawashikilia watuhumiwa wawili, mume na mke kwa kosa la kuikejeli serikali juu ya hatua zake kwenye kukabili mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Cororna.
Akiongea na waandishi wa habari leo Machi 27, 2020, Mambosasa amesema watuhumiwa hao ni Boniface Mwita (29) mkazi wa Tabata na Rosemary Mwita (41) mke wa Boniface ambao walifanya kosa hilo Machi 20, 2020.
“Watuhumiwa hao wakiwa kwenye daladala lenye namba za usajili T119 DKS wakitokea tababta kwenda hospitali ya taifa Muhimbili, walisambaza taarifa za uongo za kupotosha jamii kuhusiana na ugonjwa wa covid 19” Kamamnda Mambosasa