Wakati Serikali ikianza kufanya majaribio Treni ya Kisasa baadhi ya watu wanaoshi karibu na Reli ya SGR wamekua wakifanya uharibifu Kwa kuiba na kuharibu miundombinu hiyo jambo ambalo ni kinyume na Sheria
Mhandisi Mkazi Shirika la Reli Tanzania – TRC Stanley Wambura amesema kutokana na kuwepo Kwa changamoto hiyo shirika limeanza kampeni ya kutoa elimu Kwa wakazi wanaoishi jirani mradi huo Ili kuona umuhimu wa kutunza miundombinu
Stanley anasema wameamua kufanya mkutano na viongozi wa mtaa wa serikali Manispaa ya Morogoro Ili kutoa elimu ya uelewa kwa jamii kuhusu usalama katika reli ili kuepusha ajali, uharibifu na hujuma katika miundombinu katika maeneo ya kihonda Manispaa ya Morogoro ambapo wakazi wa maeneo hayo wametakiwa kuacha mara moja tabia ya kukata fensi na kufanya njia jambo ambalo ni kinyume cha sheria
Anasema tayari majiribio ya treni yameshafanyika kwa siku za hivi karibuni msisitizo kwa jamii ni kuacha kufanya uharibifu jambo ambalo hatari kwa usalama wao na miundombinu Kwa ujumla
Naye Polisi Jamii Reli ACP. Fadhili Ishekazoba amesema jukumu la ulinzi na usalama ni la kila mtu hivyo wananchi wanatakiwa kushirikiana Kwa pamoja na viongozi Ili kulinda mradi huo.
Kwa upande wake mwanasheria wa TRC Jonas Mahejo anasema Kwa mujibu wa sheria kwa yeyote atakayekutwa na kazia ya uharibu wa miundombinu ya reli atatozwa faini kwa kiasi cha shilingi milion 80 au kifungo cha miaka 5 jela