Ni mara chache sana tunapata takwimu kama hizi kutoka kwenye ngazi ya juu ya serikali ya Tanzania ndio maana hii stori imekua kubwa baada ya kutolewa na Waziri wa uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe bungeni Dodoma May 24 2014.
Waziri Mwakyembe amesema pamoja na ugumu wa kazi ya udereva Tanzania kuna madereva Wanawake watatu wa mabasi makubwa na Wanawake wawili wa malori ya mizigo kwenda Lubumbashi Congo.
Vilevile kuna Wahandisi Wanawake 15 wa mitambo kuongozea ndege, kuna Wanawake 8 madereva wa Treni, marubani 8 Wanawake, waongoza ndege 16 Wanawake.
Mimi ni ripota wako wa nguvu ambae kazi yake ni kuhakikisha hupitwi, kama unataka kuwa mwanafamilia wa millardayo.com na uwe unatumiwa kila taarifa kwenye mitandao ya Twitter Instagram na facebook jiunge na mimi kwenye mitandao hii kwa kubonyeza hapa >>> TWITTER INSTA FB