Watu wanne wamefariki katika ajali ya ndege iliyotokea saa chache zilizopita baada ya ndege ndogo kugonga jengo la uwanja wa ndege na kuwaka moto.
Ndege hiyo iligonga jengo la uwanja wa Wichita, Kansas Marekani na kusababisha vifo vya watu wawili waliokuwemo ndani kufariki ikiwemo rubani wa ndege, na watu wengine waliofariki waliokuwa ndani ya jengo.
Majeruhi watano katika ajali hiyo walipelekwa hospitali, watatu waliruhusiwa kutoka huku wengine wawili wakiendelea kutibiwa.
Kikosi cha askari wa zimamoto walipambana na moto huo na kuuzima ndani ya muda mfupi, na baadhi ya barabara za ndege uwanjani hapo zilifungwa japo ajali hiyo haikuathiri ratiba za ndege kutua na kuruka.
Ndege hiyo ina uwezo wa kubeba watu 13 japo idadi ya watu waliokuwemo ndani ya ndege haijafahamika, uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha ajali hiyo pamoja na thamani ya vitu vilivyoathirika kutokana na ajali hiyo.