Safari ya kumpata Rais wa TZ Mwezi October 2015 inaendelea, Majukwaa ya siasa yako busy kila mmoja anatangaza nia ya kugombea kwa wakati wake, hapa nina hiki alichokisema Waziri Steven Wasira wakati akitangaza kugombea Urais TZ jana MAY 31 2015 Mwanza.
“Nawashukuru wote kokote mlikotokea na kuja kunisikiliza, asanteni sana… Mmeacha kazi zenu na mkaja hapa ni ishara ya imani kubwa mliyonayo kutaka kujua nataka kuwaambia nini Watanzania“
“Kwa zaidi ya mwaka mzima kumekuwa na minong’ono kuhusu uwezekano wangu wa kutaka kugombea Urais wa Tanzania… Minong’ono hiyo imefanya baadhi ya watu wanifate na wengine wanishauri nigombee na wengine wamenipigia simu kunisisitizia”
“Leo nakuja Mwanza kuvunja ukimya kwa kutangaza kwamba nimekata shauri kugombea nafasi ya Urais wa Tanzania… ziko sababu zilizonifanya nigombee.. Kwanza naijua vizuri Tanzania, tangu miaka ya 1970 nimeshirikishwa katika Uongozi wa nchi yetu, nilikuwa Mbunge nikiwa na umri wa miaka 25“
Hapa akazungumzia ishu ya ubadhirifu >>> “Hakuna mtu ambaye atasamehewa kwa kuwaibia Watanzania”
Kingine alichokisema ni hiki >>> “Tumewekeza zaidi katika Miundombinu, miaka mitano inayokuja mkazo utawekwa katika Sekta zinazozalisha mali na kupambana na umaskini”>>> Steven Wasira.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.