Watoto wawili wamepoteza maisha baada ya kulipukiwa na kitu kinachodaiwa kuwa bomu katika kijiji cha Mugera, Kata ya Nyantakara wilayani Biharamulo mkoani Kagera.
Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi, amesema kuwa tukio hilo lilitokea Mei 27 mwaka huu kati ya saa 12:00 na saa 1:00 jioni, na kutaja majina ya watoto waliopoteza maisha kuwa ni Daniel Joseph mwenye umri wa miaka 14 na Charles Njola mwenye umri wa miaka 16.
Kamanda Malimi amesema kuwa watoto hao waliokuwa wakijiandaa kurejea nyumbani kutoka eneo walilokwenda kuchunga ng’ombe waliokota chuma ambacho kinadhaniwa kuwa ni bomu na bila kujua walianza kukichezea na kusabababisha kulipuka na kuwachana sehemu mbalimbali za miili yao.
DIAMOND PLATNUMZ ATINGA OFISI ZA CCM, “NIMEFARIJIKA KUONA RAIS SAMIA KAAMINI VIJANA”