Watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu 130 kwenye kituo cha Raya Islamic kilichopo Lugono Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro wanakabiliwa na changamoto ya bima yaa afya jambo ambalo linahataraisha usalama wao
Anasema kituo hicho kinategemea misaada kutoa kwa wasamalia wema kwani hakuna mfadhili hivyo changamoto hizo zinakua kikwazo kwao katika malezi Yao
Akizungunza na kituo hiki Mlezi wa kituo anayefahamika kwa jina la Raya Maganga amesema licha ya kuwepo na changamoto nyingi katika kituo hicho lakini suala.la afya limekua nalo kikwazo Kwani ukosefu wa bima ya afya inawalazimu kupoteza gharama nyingi pindi wanapopata magojwa na kufikishwa hospitali katika matibabu
Kutokana na changamoto hiyo imewalazimu hospitali ya Nanguji iliyopo Morogoro mjini kufika katika kituo hicho na kufanya huduma ya vipimo na dawa bure kwa watoto wote 130 na wasaidizi wao .
Uongozi wa hospitali hiyo unasema watoto hao wanahitaji huduma za karibu za kitabibu Kwani baadhi yao wamekutwa na magonjwa kadhaa ikiwemo ya ngozi ,meno jambo ambalo linahitaji elimj ya afya mara kwa mara waweze kujikinga na magonjwa hayo.
Dokta Nyumba Swalehe Nyumba mganga mfawidhi hospitali hiyo ya Kumbukumbu ya Nanguji anasema watoto yatima wanahitaji faraja hivyo hospitali hiyo imeguswa na kwamba Wito unatolewa kwa jamii kuendelea kuwakumbuka wenye uhitaji ili kuwasaidia.