Watu watatu wamefariki Dunia kutokana na magonjwa ya matumbo huku wengine 14 wakiugua ugonjwa huo katika Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Buhigwe Kanal Michael Ngayalina amesema hali hiyo imeanza mapema mwezi huu na chanzo kikitajwa kuwa ni wananchi kutofuata taratibu za usafi wa mazingira na chakula katika maeneo yao.