Polisi mmoja wa Michigan Marekani aitwae Cameron Maciejewski amemwagiwa pongezi nyingi mitandaoni baada ya kufanikiwa kumuokoa Mtoto wa kike mwenye umri wa wiki tatu ambaye Wazazi wake walipiga simu kuomba msaada baada ya kuona Mtoto huyo anashindwa kupumua.
Cha kwanza kilichofanya Cameron asifiwe ni kitendo cha kuwa Mtulivu na haku-panic baada ya kufika eneo la tukio, alituliza akili yake na kulitafuta tatizo kisha kulitafutia ufumbuzi ambapo alimchukua Mtoto huyo na kumsogeza kwenye mwanga pembeni ya gari na kisha kumtazama kwanza na kumgeuza na kumpigapiga mgongoni ili kuokoa uhai wake.
Sekunde chache baada ya kufanya hivyo Mtoto huyo alizinduka na kuanza kulia ambapo Cameron aliwataarifu Wazazi wake, Mama yake alikaa chini na kuanza kulia akiwa haamini kilichotokea baada ya Mtoto huyo kukabwa wakati akinywa maziwa na kumsababishia tatizo la kupumua.
Baada ya Cameron kusaidia huduma ya kwanza Mtoto huyo alipelekwa Hospitali kwa ajili ya kutazamwa zaidi, ambapo Cameron amesifiwa pia kwa kuweza kumudu kufanya kazi yake na kuituliza familia hiyo ambayo ilikua imepagawa huku Mwanamke ambaye inaaminika ndio Mama wa Mtoto akiwa analia wakati wote, unaweza kutazama video ya tukio hapa chini.
MAAJABU: DUKA LISILO NA MLANGO WA MBAO WALA WA CHUMA NA HAKUNA ANAYETHUBUTU KUDOKOA CHOCHOTE, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA