Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa amewatoa hofu Watanzania kutokana na kupanda kwa bei ya sukari na kusema nchi imeagiza tani zaidi ya elfu 20 kutoka nje kama tahadhari ya kuwa na akiba katika kipindi hiki cha ugonjwa wa COVID-19.
Akizungumza na wanahabari jijini Dodoma, Mhe. Bashungwa amesema serikali inafanya jitihada za kuongeza uzalishaji wa sukari huku ikiwa imeunda tume ya wataalamu ili wafanyabiashara watakaobainika kuficha sukari wachukuliwe hatua kali.
Waziri Bashungwa amesema kuwa tayari sukari iliyokwisha ingia bandarini kupitia kampuni ya Kagera Sugar ni Tani 9,990 na imeanza kutolea bandarini tangu jana jioni.