Waziri wa Kazi na Usafirishaji wa Uganda, Jenerali Katumba Wamala amenusurika kuuwawa katika shambulio la risasi katika gari lake. Picha zilizosambaa katika mitandao ya kijamii zimemuonyesha Jenerali Katumba akiwa nje ya gari huku nguo ikiwa imetapakaa damu huku gari likiwa na matundu ya risasi.
Msemaji wa jeshi la Uganda amesema katika shambulio hilo Jenerali Katumba amejeruhiwa wakati binti yake na dereva wakipoteza maisha.
Shambulizi hilo limetokea katika kitongoji ambacho mwaka 2017 watu wenye silaha wakiwa kwenye pikipiki walishambulia gari la kiongozi wa juu katika jeshi la polisi ambaye aliuwawa.