Waziri mkuu nchini Italia Giuseppe Conte amesaini pendekezo la kamati ya Olympic nchini Italia la kutaka michezo yote Italia ikiwemo Serie A kusimama kwa muda kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.
Kwa sasa Italia imeripotiwa kuwa Ligi Kuu ya Italia Serie A ni waathirika pia wa maamuzi hayo, Serie A imesimamishwa hadi April 3 2020.
“Eneo lote la Italia linalindwa na kufungwa Ligi zote zitasimama na Rais wa mikoa yote Italia amekubaliana na maamuzi haya, pole kwa mashabiki wote Serie A pia inabidi isimame”>>> Conte