Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ametangaza kupungua kwa idadi ya wagonjwa wa COVID 19 wanaoendelea na matibabu katika Hospitali na Vituo vya Afya maalum vilivyotengwa katika mikoa ya Dar es salaam, Pwani na Dodoma ambapo wagonjwa waliobaki ni 32 katika mikoa hiyo.