Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa Kassim amesema Kituo cha reli ya kisasa SGR cha Tanzanite jijini Dar es Salaam kimekamilika kwa asilimia 100 ambapo kufikia August 2021 treni itaanza kazi kuanzia Morogoro hadi Pugu Dar es Salaam.
Waziri Majaliwa ameyasema hayo leo wakati alipofanya ziara ya mradi huo kuanzia kwenye Kituo hicho cha awali cha treni ya Tanzanite jijini Dar es Salaam. “Hata majirani watakuja kujifunza hapa wao wanaiita ya Diesel sisi ya umeme watakuja kujifunza hapa,” Waziri Mkuu Majaliwa.