Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli, amewataka Watanzania kuacha kutiana hofu na badala yake wawe na umoja yanapotokea matatizo, hii ni baada ya mitandao ya kijamii kuzusha kwamba Waziri wa Fedha Dkt. Philip Mpango, amefariki dunia taarifa ambazo amezikanusha.
“Tumefikia mahali sasa tunatishana sana, leo nilitumiwa meseji na Waziri wa Fedha Dkt. Mpango, ambaye amelazwa Dodoma, na ninaomba niusome hapa kwa faida ya wale ambao walikuwa wana-Tweet kwamba amekufa na amenitumia leo asubuhi”, Rais Dkt. Magufuli
“Ameniambia Rais asante sana nimepata ujumbe wako kupitia kwa mke wangu, kwa Neema ya Mungu naendelea vizuri, nakula na ninafanya mazoezi ya kifua na kutembea hao wanaonizushia kifo niliwaombea msamaha kwa Yesu wakati wa sala ya jioni jana, Mungu akubariki na akupe Neema na ujasiri zaidi katika kuliongoza Taifa letu katika wimbi hili” JPM