Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametoa hotuba Bungeni leo kuhusu Makadirio ya mapato na matumizi ya Fedha ya Wizara ya Afya 2022/2023
Ambapo amesema “Katika kipindi cha July 2021 – Machi, 2022, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imehudumia Wagonjwa 367,213, kati ya hao, wa nje (OPD) walikuwa 328,938 na wa kulazwa (IPD) 38,275, Wagonjwa wa misamaha walikuwa 46,591 ambao waliigharimu Hospitali Tsh. Bilioni 14.1”- Waziri Ummy
“Katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022, Hospitali imetoa huduma ya upandikizaji figo kwa Wagonjwa 6 ambapo gharama ya huduma hiyo ni Tsh. Milioni 30 kwa mmoja ambapo huduma hiyo hugharimu Tsh. milioni 120 nchini India, waliopandikizwa figo tangu huduma hiyo ilipoanzishwa nchini mwaka 2017, wamefikia 70, hivyo Wagonjwa 70 waliopata huduma hii Muhimbili wangegharimu Tsh. 8,400,000,000 iwapo wangepata huduma hiyo India, kwa kuanzisha huduma hii nchini Serikali imeokoa Tsh. 6,300,000,000”- Waziri Ummy Mwalimu
“Katika kipindi cha Julai 2021 mpaka Machi, 2022, Hospitali imetoa huduma ya upandikizaji vifaa vya usikivu kwa Watoto 14 ambapo gharama ya huduma hiyo ni Tsh. Milioni 36 kwa Mgonjwa mmoja ambapo huduma hiyo hugharimu Tsh. Milioni 100 nchini India, Wagonjwa waliopandikizwa vifaa vya usikivu tangu huduma ilipoanzishwa nchini 2017, wamefikia 49 kwa gharama ya Tsh. Bilioni 1.764, hivyo Watoto 49 waliopata huduma hii Muhimbili wangegharimu Tsh. bilioni 4.9 Kwa kuanzisha huduma hii hapa nchini Serikali imeokoa jumla ya shilingi bilioni 3.136”- Waziri Ummy Mwalimu
ULIKOSA ALICHOKIFANYA ZARI THE BOSS LADY KWENYE USIKU WA JUX KIDIMBWI BEACH, BASI ITAZAME HII VIDEO HAPA