Mix

Watuhumiwa wengine Sita wa Ujambazi wauawa na Polisi Mwanza

on

Miongoni mwa habari zilizosomwa usiku wa July 8, 2018 kwenye Televisheni za Tanzania ni pamoja na hii iliyoruka kupitia Channel 10 ambapo Jeshi la Polisi Mwanza limeaanza kuvunja mtandao wa majambazi wanaofanya uhalifu nchini ikiwemo mauaji yanayoendelea Kibiti.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi amesema Jeshi la Polisi limewaua majambazi sita kati ya wanane wakati wa majibizano ya risasi na Polisi huku wawili kati yao walikimbia huku Jeshi hilo likifanikiwa kukamata silaha za kivita, mavazi ya kijeshi, pamoja na nyenzo mbalimbali za kufanyia uhalifu.

>>>”Tutamkamata mmoja baada ya mmoja. Kitu ambacho tunataka kuwaambia waache kufanya uhalifu wasome alama za nyakati. Ukifanya ubaya utalipwa kwa ubaya. Sisi tupo wengi wao wapo wachache.” – RPC Ahmed Msangi.

VIDEO: Mtanzania aliyekataa mshahara wa Tsh. 425m Marekani amerejea nchini

Soma na hizi

Tupia Comments