Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Rais wa Real Madrid ameguswa na kifo cha staa wa Arsenal, ameahidi hili kwa mtoto wa marehemu

on

Kifo cha ajali ya gari cha mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania aliyewahi kuvichezea vilabu mbalimbali Ulaya kama Arsenal, Sevilla na Real Madrid Jose Antonio Reyes kimewagusa watu wengi wa soka, taarifa za kifo cha mchezaji huyo kimewashitua wengi kutokana na kutokea ghafla.

Reyes mauti yalimkuta June 1 Hispania katika ajali ya gari lake binafsi, hivyo kutokana na kuacha mtoto mdogo mwenye umri wa miaka 11, Rais wa club ya Real Madrid Firentino Perez ameripotiwa kuwa ameahidi kumlea mtoto wa Reyes kwa kila kitu hadi afikie umri wa miaka 18.

Reyes

Kwa sasa ana miaka 11 ana alikuwa katika academy ya Leganes ila kuanzia msimu ujao Real Madrid watamchukua na kumuhamishia katika academy yao, ikiwa ni sehemu ya malezi ya Perez kwa mtoto huyo ambaye alikuwa bado anahitaji malezi ya baba yake aliyepoteza maisha akiwa na umri wa miaka 35, game ya mwisho ya Reyes kucheza ilikuwa May 18 akiichezea timu yake ya Extremadura ya Segunda Division (daraja la pili).

EXCLUSIVE: Msuva kuhusu kitendo cha Salamba kuomba viatu vya Banega

Soma na hizi

Tupia Comments