Kocha wa klabu ya Arsenal ya Uingereza Arsene Wenger ambaye amewahi kumfundisha Thierry Henry kama mchezaji wake kwa miaka mingi, Wenger amemshauri Thierry Henry kama kweli ana nia ya dhati ya kutaka kupata mafanikio kama kocha katika soka.
Wenger amemshauri Henry ambaye kwa sasa anaifundisha timu ya Arsenal chini ya umri wa miaka 18 kuwa, kama kweli anataka kupata mafanikio katika ukocha inabidi apate ushauri wa kisaikolojia katika akili yake. Henry anafundisha kikosi hicho cha vijana huku akipata mafunzo ya ukocha.
Henry ambaye anaheshima ya kuwa mfungaji bora wa klabu ya Arsenal kwa muda wote, alisajiliwa na Wenger akitokea klabu ya Juventus ya Italia mwaka 1999 ila Wenger amemueleza utofauti uliyopo kati ya kuwa mchezaji na kuwa kocha.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos