Tunayo stori kutokea kwa Wakala wa Usajili, Udhamini na Ufilisi (RITA) ambapo imeeleza kuwa moja kati ya vielelezo vinavyotakiwa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kwa wanafunzi wanaoomba mikopo ni uthibitisho wa vyeti vyao vya kuzaliwa.
Akizungumza na waandishi wa habari, Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Emmy Kalomba amesema lengo la uthibitisho huo ni kuhakikisha wanafunzi wanaostahili kupata mikopo waweze kupatiwa.
“Mwaka jana RITA ilifanya zoezi kama hili na zaidi ya waombaji Laki Moja waliwasilisha maombi yao kwa ajili ya kuhakikiwa na kati ya hao Elfu Kumi na Nane na nyaraka zao zilikuwa halali,“amesema.