Spika wa Bunge la Afrika Kusini Baleka Mbete amesema hotuba ya kila mwaka ya Rais Jacob Zuma ambayo ingeelezea kuhusu hali ya nchi, imeahirishwa kutokana na mashinikizo anayokabiliana nayo Rais huyo.
Hotuba hiyo ilikuwa isomwe na Zuma kesho February 8, 2018 bungeni lakini sasa imeahirishwa hadi wakati mwingine huku rais huyo akiendelea kushinikizwa ajiuzulu.
Afisa mmoja wa ngazi ya juu katika chama tawala nchini Afrika Kusini (ANC) amesema kuwa Zuma anapaswa kujiuzulu na hivyo kuzidisha mashinikizo dhidi ya rais huyo ambaye anaonekana kudhoofika kisiasa tangu Makamu wake wa Rais Cyril Ramaphosa achaguliwe kuwa Mwenyekiti wa chama tawala ANC December 2017.
MAWAZIRI MPUNGUZE MEHEMKO, MNAWAUMIZA WANANCHI” -MBUNGE MUSUKUMA