Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo amekerwa na ufisadi uliofanyika kwenye ujenzi wa Kituo cha Afya cha Mtande katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya uliofanywa na baadhi ya wasimamizi wa Serikali.
Kituo hicho ni miongoni mwa vituo 14 vya Afya ambavyo vinajengwa na Serikali kwa kushirikiana na wananchi mkoani Mbeya kupitia mfumo wa akaunti ya dharura (Force account) ambao unahamasisha matumizi ya mafundi wa mitaani badala ya wakandarasi.
Akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Waziri Jafo aliagiza vyombo vya dola kuwashughulikia ipasavyo wote watakaobainika kuhusika na ufisadi huo baada ya tume iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa kuchunguza mradi huo kukamilisha kazi.
Amesema taarifa zinaonyesha kuwa kuna vifaa vingi vya mradi huo vimechakachuliwa na hivyo kuufanya kuchelewa kukamilika na hata ubora wake ni wa wasiwasi tofauti na vituo vingine vilivyojengwa mkoani humo kikiwemo cha Chalangwa.
Amesema mafisadi hao walitumia mwanya wa kilipo kituo hicho kutofikika mara kwa mara na viongozi kutokana na umbali, kuhujumu mradi ambapo alisema umbali wa zaidi ya kilomita 90 kutoka Chunya mjini.
AFISA MADINI APEWA SIKU MBILI “ZINAHITAJIKA TAARIFA RASMI ZA MGOGORO”