Katibu Mkuu wa shirikisho la soka Tanzania TFF Wilfred Kidao amelizungumzia suala la golikipa wa Yanga Ramadhani Kabwili kudai kuwa Simba SC iliwahi kumshawishi ajipatishe kadi ya tatu ya njano ili akosekane katika mchezo vs Simba SC kwa kufanya hivyo angepewa Toyota IST kama hongo.
TFF jana ilitoa tamko na kuanza kuzifanyia uchunguzi shutuma za golikipa huyo kudai kuwa aliahidiwa na mmoja kati ya viongozi wa Simba ili ajitafutie kadi ya 3 ya njao katika mchezo dhidi ya JK Tanzania kwa makusudi ili akose mchezo uliokuwaunafuata vs Simba.