Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imesema Serikali imekuwa ikichukua hatua bila kupendelea chombo chochote cha habari kinachobainika kukiuka Sheria na taratibu ikiwamo kutoa habari za uongo.
Naibu Waziri, Juliana Shonza ameyasema hayo baada ya Mbunge wa Konde, Khatib Said Haji (CUF) kudai kuwa ameshuhudia baadhi ya vyombo vya habari, hususan Magazeti yakipewa adhabu ya kufungiwa kwa kutoa habari za uongo, lakini kuna ambayo hayachukuliwi hatua zozote pamoja na kwamba yanadhalilisha na kuchafua watu.
Shonza amesema suala hilo halina ukweli kwa kuwa Serikali inafanya kazi kwa kusimamia Sheria na Kanuni zilizopo na Sheria ya Habari inaeleza kwamba kabla ya kuchukua hatua yoyote kwa chombo cha habari, kwanza wanapaswa kupewa onyo.
Amesema si kweli kwamba hawachukui hatua kwa Magazeti ya Tanzanite kwani wameshawaandikia onyo pamoja na mengine yaliyokuwa yanakiuka Sheria na hatua hizo zimekuwa zikichukuliwa bila upendeleo.
SERIKALI YABUNI UTARATIBU MPYA WANAFNZI WA MADINI KUFUNDISHWA NCHINI