Kumekuwa na taarifa zinazosambaa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu tetesi za uwepo wa raia wa kigeni katika Mkoa wa Dar es Salaam anayeshukiwa kuwa na dalili za ugonjwa wa virus vya Corona.
Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Mamlaka husika ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam umefuatilia ukweli wa taarifa hizo na kubaini kuwa kuna raia wa kigeni (jina limehifadhiwa) mwenye asili ya China aliye wasili nchiniFebruari 2, 2020 akitokea Jamhuri ya Watu wa China ambaye alishukiwa kuwa na dalili za ugonjwa wa Corona.
Timu ya wataalamu wa Afya ilifika eneo analoishi mshukiwa (eneo limehifadhiwa) na kufanikiwa kumfanyia uchunguzi ambapo ilibaini kuwa raia huyo wa kigeni hana dalili (homa, maumivu ya kichwa, mafua na maumivu yoyote ya mwili) za kuwa na maumivu ya Corona.