March 4 2014 msemaji wa kampuni ya WEUSI Nikki wa II aliongea na AyoTV na kukiri ‘ni kweli kampuni ya WEUSI imemsimamisha Lord Eyez kikazi kwa sababu kila kampuni duniani ina misingi yake ya kazi, sababu za kumsimamisha ni nyingi ila mojawapo ni utovu wa nidhamu ambapo anaesimamishwa kwenye kampuni hatohusika na chochote cha kundi zikiwemo Project, lakini tutakua na vikao vyetu kuangalia itakuaje’
Toka uamuzi huo wa kumsimamisha ulipotangazwa, Jumapili ya May 25 2014 ndio imekua mara yangu ya kwanza kumuona Lord Eyez akiwa kwenye picha ya pamoja na Joh Makini ambae ni mmoja wa wakali kutoka kampuni ya WEUSI ambayo wengi waliamini hawaelewani kabisa wala kukutana na Lord Eyez toka alipoadhibiwa.
Kwenye picha iliyopigwa kwenye birthday party ya mshkaji wao Arusha May 25 2014, Joh Makini aliandika upendo ndio kila kitu na my fam Lordize.
Mpaka hii post inachukuliwa kwa Joh Makini saa tisa na dakika kumi na moja usiku wa May 25 2014, kulikua na comments za watu 20 waliokua wameandika vitu mbalimbali ambapo comments 8 kati ya hizo zilimtaja Lord Eyez pekee bila kuhusisha kingine chochote kwenye post hiyo iliyohusu birthday party.
Ukiwa kama shabiki wa WEUSI, umemmis Lord Eyez? unawaambia nini WEUSI kuhusu kumrudisha? kama pia una kingine chochote niachie hapa chini na kitawafikia wenyewe leo jioni.
Unapenda stori kama hizi zisikupite? niko tayari kukutumia wakati wowote mtu wangu, jiunge na mimi kwa kubonyeza >>> Twitter Instagram facebook na kupata pichaz, video, stori na mengine yote ya hii dunia.