Bodi ya Filamu Tanzania inatarajia kuwakutanisha wadau wa sekta ya Uigizaji wakiwemo viongozi wa dini kwa ajili ya kuwajengea uwezo waigizaji pamoja na kutambua thamani zao.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Katibu Mtendaji wa Bodi hiyo, Joyce Fisso amesema watashirikiana na Chama cha Waigizaji ambapo watazungumzia mambo mbalimbali katika mkutano huo.
Amesema miongoni mwa mambo yatakayozungumzwa ni jinsi waigizaji watakavyojitangaza na kuongeza thamani zao, pia nafasi ya muigizaji katika uzalishaji wa filamu bora, kufanyakazi kwa uweledi pamoja na haki na makubaliano hasa kwa kupatiwa mikataba.