Mwaka 2015 unakaribia kuisha na baadhi ya watu wameshaanza kufanya mipango yao watakachokifanya mwaka 2016. Kwa mwaka 2015 Wema Sepetu ametajwa mara kadhaa kutokua na maelewano na baadhi ya marafiki zake wa zamani ikiwemo Kajala, pia kuendeleza uhusiano mzuri na watu aliokua hapatani nao zamani kama Penny.
Kwenye moja ya mipango ya Wema Sepetu kwa mwaka 2016 ameweka wazi kwamba yeye hana mpango wa kuanza mwaka akiwa na beef na mtu yoyote… Wema amesisitiza kwamba anaomba watu wote aliowakosea kwa mwaka 2015 wamsamehe na yeye anawasamehe wote waliomkosea.
Maneno ya Wema Sepetu kwenye post yake @Instagram yanasomeka hivi >>> “Mi nataka mwaka unapoanza inshallah tukijaaliwa nisiwe na beef na mtu yoyote wala kiumbe yoyote… Kwa wale nilowakosea na walionikosea …. Nasema Im sorry….. Life Goes On…. We all live to make mistakes…. Ama nene…. ???? And I thank everyone for making me the person Iam TODAY….“>> @wemasepetu
Hivi karibuni Wema alizindua lipstick zake zinaitwa ‘Kiss by Wema Sepetu‘ pia alifanya movie akiwa na mwigizaji Van Vicker wa Ghana na bado haijatoka.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.