Ni kiasi siku kumi sasa tangu tukio la kuvamiwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kisha kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi na watu wasiojulikana Mchana wa September 7, 2017 akiwa nyumbani kwake Area D, Dodoma muda mfupi baada ya shughuli za Bunge.
Tangu hapo watu mbalimbali kutoka kada tofauti wamekuwa wakilielezea tukio hilo kwa namna hisia kali wengi wakitaka ufanywe uchunguzi wa kina ikiwezekana kushirikisha Jamii za Kimataifa kuhakikisha waliotekeleza tukio hilo wanajulikana na wanakamatwa ili sheria ifuate mkondo wake.
Miongoni mwa watu hao ni pamoja staa kutokea Bongoflevani Wakazi ambaye amekaa na Ayo TV na millardayo.com na kufunguka kuelezea hisia zake namna alivyoguswa na tukio la Lissu kushambuliwa huku akitaka wahusika wasakwe.
TAMKO LA BAVICHA BAADA YA TUNDU LISSU KUPIGWA RISASI
TAMKO LA CHADEMA KUHUSU KUSHAMBULIWA KWA RISASI TUNDU LISSU