Jumatano October 11, 2017 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeutaka upande wa mashtaka kuhakikisha unafika na mashahidi katika kesi ya uhujumu uchumi wa kujihusisha na biashara ya Meno ya Tembo yenye thamani ya Tsh. Bilioni 13 inayomkabili raia wa China, Yang Feng Glan na wenzake.
Mbali ya Glan maarufu kama Malkia wa Meno ya Tembo, wengine ni Philemon Manase na Salvius Matembo.
Wito huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Wakili wa Serikali, Elia Athanas kudai kesi imekuja kutajwa anaomba tarehe nyingine ambapo baada ya kueleza hayo, Wakili wa utetezi, Nehemiah Nkoko aliuomba upande wa mashtaka uje na mashahidi katika tarehe ijayo.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi October 17, 2017 ambapo itasikilizwa mfululizo hadi October 20, 2017, huku Hakimu Shaidi akiutaka upande wa mashtaka kufika na mashahidi.
Katika kesi ya msingi, washtakiwa kwa pamoja wanakabilia na kesi ya uhujumu uchumi kwa kujihusisha na biashara ya Meno ya Tembo yenye thamani ya Tsh Bilioni 13 ambapo wanadaiwa kuwa kati ya January Mosi, 2000 na May 22, 2014 walijihusisha na biashara ya nyara za Serikali.
Katika kipindi hicho washtakiwa hao wanadaiwa kufanya biashara ya vipande 706 vya meno ya Tembo vyenye uzito wa kilogramu 1,889 zenye thamani ya Th Bilioni 5.4 bila ya kuwa na leseni iliyotolewa na Mkurugenzi wa Wanyama Pori.
KILIMANJARO: Polisi wamuua jambazi sugu, kakutwa na simu 19 na line 58
DIWANI MWINGINE KAWAJIBU LEMA NA NASSARI, KATOA SIKU SABA