Jina lake ni Injinia Chacha Wambura ambae ni Mkurugenzi wa shule za Waja ambae leo ameamua kuweka wazi kwanini ametoa zawadi za gari kwa Wanafunzi waliofanya vizuri kitaifa.
“Kwanini hatukumpa hela, kumlipia ada au kufanya kitu kingine na sio kumpa gari, Mwanafunzi mwenyewe anakwambia kitu atachokifurahia na kuona amejaliwa ni zawadi ambayo inakwenda moja kwa moja kwake ambayo ni gari“
“Pamoja na kumzawadia hilo gari, shule za Waja tutasimamia gari lake kwa mwaka mzima kuanzia kwenye mafuta, BIMA, kuwalipia service ya gari na hata kuwalipia watoto kusomea Udereva…. zawadi kubwa sio lazima itolewe kwa Mamiss peke yake” – Injinia Wambura.
Unaweza kutazama zaidi hapa chini ili kupata maelezo ya kutosha.