RAIS wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania, Jaji Ignas Kitusi amewataka Majaji na Mahakimu kufuata sheria, miiko na maadili ya utendaji wa kazi zao huku akiitaka Serikali kuiwezesha Mahakama kifedha katika bajeti yao ili iweze kutekeleza majukumu yake na kuamua kesi kwa haraka.
Jaji Kitusi ameyasema hayo wakati wa kufunga mkutano wa Majaji na Mahakimu wa Jumuiya ya Madola uliofanyika Dar es Salaam kuanzia September 25 na kufungwa leo September 27, 2017.
Aidha, amesema, jamii inatakiwa kuiacha Mahakama iweze kufanya kazi yake sambamba na Serikali kuhakikisha usalama wa Mahakimu na Majaji ili waweze kuamua kesi vizuri.
>>>”Katika mkutano huu tumejadili mambo mbalimbali ikiwemo changamoto ya mitandao, masuala ya ulinzi katika nchi zetu pamoja na biashara ya binadamu.”
Alisema wamezungumzia changamoto ya ucheleweshwaji wa mashauri, kifedha na rasilimali watu ambavyo vyote vinahitaji ushiriki wa Serikali.
Naye Waziri wa Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Zanzibar, Haroun Ali Suleiman kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein alisema Mahakama zina mchango mkubwa katika maendeleo.
Alisema madhumuni ya mkutano huo ni kujengeana uzoefu, kupambana na ucheleweshwaji wa kesi na kwamba si vizuri kwa mihilili kuingiliana.
Aidha, Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Makungu alitoa wito kwa Majaji na Mahakimu kufanya kazi kwa misingi ya sheria kwa sababu sheria imewapa meno.
ULIPITWA? Taarifa aliyoitoa Jaji Mkuu wa Tanzania kwa wanahabari
Jaji Mkuu kajibu kuhusu kulinganisha uhuru wa mahakama kati ya TZ na Kenya