Top Stories

Wahamiaji 90 wanahofiwa kuzama Bahari ya Mediterania

on

Wahamiaji zaidi ya 90 wanahofiwa kuzama maji nchini Libya baada ya boti yao kuzama siku ya Ijumaa February 2, 2018.

Taarifa ambayo imetolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wahamiaji limeeleza kuwa boti hiyo ilikuwa ikipita njia ambayo kwa kawaida huwa inatumiwa na maharamia kwenda Italia kupitia Bahari ya Mediterania.

Tayari watu watatu wamesharipotiwa kunusurika baada ya kuogelea hadi ufukweni na miili 10 tayari pia imetokea kwenye ufukwe ambapo nane kati yao imetambuliwa kuwa Wapakstani na wawili Walibya.

Alichokiongea Edy Kenzo jinsi alivyoguswa na msiba wa Radio

Soma na hizi

Tupia Comments