Top Stories

Ushahidi uliotolewa Mahakamani kesi ya Wema Sepetu Sept 12

on

Leo September 12/2017 Ofisa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Inspekta Wille ameiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa alikuta msokoto wa Bangi kwenye Kabati la Vyombo la Wema Sepetu.

Inspekta Wille ameyaeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati akiongozwa na wakili wa serikali, Constantine Kakula kutoa ushahidi katika kesi ya dawa za kulevya inayomkabili Wema na wenzake.

Hata hivyo, wakili wa utetezi Peter Kibatala alipinga kupokelewa kwa hati hiyo, akidai ina mapungufu kisheria na kutokana na mvutano huo, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi September 13/2017 kwa ajili ya kutoà uamuzi wa kupokea au kutopokea kielelezo hicho.

Uliiona hii? GUMZO JINGINE LA MANJI: Ni kuhusu Udiwani Mbagala Kuu

Hii je? Mawakili wataka sheria ya Wakuu wa Mikoa kufunga watu saa 48 ifutwe

Soma na hizi

Tupia Comments