Leo September 20, 2017 Upande wa utetezi umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa kesi ya utakatishaji fedha Dola za Marekani Milioni 6 inayomkabili Kamishna Mkuu wa zamani TRA, Harry Kitilya na wenzake imechukua mwaka mmoja na nusu bila upelelezi kukamilika.
Mbali ya Kitilya washtakiwa wengine ni aliyekuwa Miss Tanzania mwaka 1996, Shose Sinare na Sioi Solomon.
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi amemueleza Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha kwamba wanaomba wapangiwe tarehe nyingine kwa sababu wameshindwa kufanyia kazi upelelezi wa kesi hiyo kwa muda waliiomba.
Baada ya kueleza hayo, Wakili wa utetezi Masumbuko Lamwai amedai kwa mujibu wa hati ya mashtaka, kesi hiyo ilifikishwa Mahakamani hapo April 1, 2016.
>>>”Huu ni mwaka mmoja na nusu sasa upelelezi bado, tena ukiangalia makosa yanayowakabili washtakiwa ni dhahiri yanatokana na nyaraka ambazo upande wa mashtaka unazo, ndio maana tulivyoenda Mahakama Kuu tulisema hii kesi ni ya kukomoana.”
Aidha, Lamwai amedai kuwa washtakiwa ni watu wazima, wana familia na biashara ambazo nyingine zinafilisika na kuiomba Mahakama itambue Jamhuri wanaitumia vibaya Mahakama.
>>>”Naomba Mahakama itambue kwamba Jamhuri wanaitumia vibaya Mahakama.”
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mkeha aliutaka upande wa mashtaka na washtakiwa wawe wavumilivu kwa sababu, anaamini upelelezi unafikia mwisho>>>”Nimeshuhudia kwa macho na nimejiridhisha kuhusu nyaraka za upelelezi, hivyo nawaomba muwe na subira.”
Hakimu Mkeha ameahiriaha kesi hiyo hadi October 5, 2017.
“Inawezekana Mungu alikosea kuweka Tanzanite kwa Watanzania” – President JPM