Club ya Yanga SC leo ilikuwa Mwanza katika uwanja wake wa nyumbani wa muda wa CCM Kirumba kucheza mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2018/2019 dhidi ya African Lyon, Yanga wametumia uwanja wa CCM Kirumba kutoka na uwanja wa Taifa kusimamishwa kutumika kwa sababu za kusubiri michuano ya AFCON U-17 2019.
Yanga wakiwa katika uwanja huo wameendelea kujichimbia kileleni kufuatia kupata ushindi wa magoli 2-0, magoli ya Yanga yakifungwa na mshambuliaji wao raia wa Congo Heritier Makambo dakika ya 5 na 32 ya mchezo na kuihakikishia Yanga point tatu muhimu zinazowafanya wajikite zaidi kileleni, huku African Lyon ikididimia katika nafasi ya mwisho kwa kuwa na point 22 na wamebakiza michezo 5
Ushindi huo wa Yanga leo umewafanya waendele kuongoza TPL lakini wakiwaacha African Lyon katika hali mbaya, Yanga anaongoza TPL kwa kuwa na point 71 akicheza michezo 30 na kubakiza 8, Azam FC anafuatia kwa kuwa na point 63 akicheza michezo 3o, Simba nafasi ya tatu kwakuwa na point 57, akicheza michezo 22, viporo michezo 8 na amebakiza michezo 8 kumaliza Ligi.
“Nina uhakika tunaweza kushinda Lubumbashi na kufuzu”- Kocha Simba SC